2:53 PM

Rihanna, Chris Brown Kwa Siri wakutana kwenye Yacht Na Kuparty Mpaka Asubuhi

Chris Brown, Rihanna
Chris Brown na Rihanna

St. Tropez, France Jumapili.

Gazeti mashuhuri la Us Weekly limedai kwamba wale waliokua mahasimu wakubwa, ambao waliachana mwaka 2009 baada ya Brown kupatikana na hatia dhidi ya aliyekua girlfriend Rihanna, wiki iliyopita walipata njia ya kukutana kwa siri.
Mwimbaji huyo wa nyimbo ya "Where Have You Been?", 24, inadaiwa alipojua Chris atakuja Ufaransa ilibidi abadili ratiba na kusubiria huko huko.

"Rihanna alijua Chris alikua njiani kuja Ufaransa [St. Tropez] na akabadili plani zake siku ya Ijumaa baada ya kumpigia Chris simu na kukubaliana waonane," chanzo kilidai Us.

Brown, 23, amekodi boti la kifahari, likiwa na swimming pool na sehemu maalum ya kutua helkopta mbili. Mwimbaji huyo wa "Turn Up the Music" inasemaeka amekodi boti hilo la kifahari na Swizz Beatz pamoja na  Ludacris -- kwa kiasi cha $400,000 kwa wiki -- kwa ajili ya kushuti video mpya.
"Rihanna alikwenda na kukesha huko na majamaa ndani ya boti," chanzo kilisema.

Karrueche Tran akitoka kufanya shopping

Chanzo kingine kimedai kwamba girlfriend wa sasa wa Brown, Karrueche Tran, pia alikuwepo kwenye boti ila kutokana na ukubwa wa boti lenyewe kati yao hakuna hata aliyejua kama mweza wake yupo humo. "Sijui kama Rihanna alijua kama Karrueche Tran alikuwepo!"
Ingawa Rihanna na Brown wamekua wakijitahidi wasionekane hadharani pamoja, iliwashangaza watu pale RIRI alipoamua kumshirikisha Chris kwenye remix ya nyimbo yake ya "Birthday Cake."

"Sikudhani kama watu wataongea kuhusiana na hili," aliliambia jarida la Esquire UK mwezi June. "nilidhani watu wangefurahia kusikia tunarekodi pamoja, sikudhani kama watu wanaweza ona kama tulichofanya si kizuri. Kwa nionavyo mimi ni muziki tu . . . Nisingeweza ona ubaya kufanya nae muziki."

Je wadhani wamerudiana?

0 comments

Leave a reply

Posts Mpya

Comments Zenu

Hapa