Showing posts with label blog. Show all posts
Showing posts with label blog. Show all posts
9:49 PM

Goal-line Technology Kuanza Premier League

TEKNOLOJIA ya kuthibitisha kama mpira umevuka msitari na kuingia wavuni, inayofahamika kama ‘Goal-line technology’, huenda ikatumiwa katikati ya msimu wa ligi kuu ya Premier ya England, ya mwaka 2012 hadi 2013, baada ya utaalamu huo kuidhinishwa na halmashauri ya kimataifa ya mchezo wa kandanda, IFAB, Alhamisi, mjini Zurich. Teknolojia mbili ziliidhinishwa, moja ikifahamika kama ‘Hawk-Eye’, yaani ‘jicho la mwewe’, na ya pili inafahamika kama ‘GoalRef’, ikimaanisha ‘mwamuzi wa goli’.


Mbinu mbalimbali za kuhakiki kuvuka kwa mpira langoni bado zinafanyiwa utafiti.


 Teknolojia hiyo kwa mara ya kwanza itatumiwa katika michuano ya Kombe la Dunia la vilabu vya soka mwezi Desemba, na iwapo itaonekana inafaa, basi itatumiwa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho mwaka 2013, na vile vile katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.


Dhahiri John Terry akiokoa mpira uliokwisha pita lango.


  Mbinu hiyo ya ‘jicho la mwewe’ inafanya kazi vipi?


Utaalamu huu unategemea kamera sita, zikiangazia kila lango, na kuufuata mpira uwanjani. Kisha kiufundi, huwa teknolojia inatambua mahali halisi mpira ulipo, kupitia utaalamu unaojulikana kama ‘triangulation’. 


Ikiwa mpira utavuka msitari wa goli, basi ujumbe kupitia mawimbi ya redio hutumwa moja kwa moja hadi katika saa ya mkononi aliyovalia mwamuzi, kumwarifu kwamba bao limefungwa. 


Kama kanuni za FIFA zinavyohitaji, utaratibu mzima hauchukui zaidi ya sekunde moja. Teknolojia ya ‘GoalRef’ nayo hutumia kifaa kinachojulikana kama ‘microchip’, ambacho hubandikwa katika mpira unaotumiwa, na kwa kutumia mawimbi ya smaku karibu na goli. Iwapo mabadiliko funali yatajitokeza katika mawimbi kupitia mpira kuvuka msitari, teknolojia inaamua kama hilo ni goli, na kisha kwa njia ya elektroniki, mwamuzi hujulishwa katika muda wa sekunde moja kwamba goli limefungwa.


Si kazi rahisi kama tudhaniavyo:Inatia shaka kwa nchi changa kiuchumi kumudu gharama za vifaa hivyo.


 Wasimamizi wa ligi kuu ya Premier wamesema wanataka kuanza kuitumia teknolojia hiyo mpya haraka iwezekanavyo. Katika mkuu wa chama cha soka cha England, Alex Horne, amesema ni wajibu wa wasimamizi wa ligi kuu ya Premier kuamua ni lini wangelipenda kuanza kuitumia teknolojia hiyo mpya.


“Tayari tuna teknolojia ya Hawk-Eye katika uwanja wa Wembley, kile kinachohitajika tu ni kuiweka sawa na kuhakikisha inafanya kazi vizuri na kuidhinishwa kwa leseni, na kwa hiyo tumekaribia sana kukamilisha matayarisho yetu katika kuitumia teknolojia hiyo. 


“Kombe la FA huenda likatufanyia uamuzi, kwa kuwa tunaweza kuitumia katika nusu faianli na fainali za FA, na sidhani huo ni uamuzi ambao utata.” Horne aliongezea kwamba anahisi “hii ni siku muhimu sana” kwa kandanda.
8:18 PM

Sasa Mtu kujipima UKIMWI mwenyewe

MAREKANI imetangaza kuwa inaruhusu kuuzwa kwa chombo cha kupima virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa binaadamu vya HIV. Chombo hicho sawa na kijisanduku kidogo kitawasaidia Wamekani kujipima wenyewe HIV majumbani . 


Badala ya utaratibu wa sasa wa kwenda hospitalini na katika vituo maalumu vya Afya kutambua afya zao. Kiongozi wa Mamlaka ya Chakula na dawa wa taifa hilo (FDA) na Kampuni iliyofanikisha kutengeza kikasha hicho ya OraSure Technologies cha kupima virusi vya HIV1 na HIV2, kwa pamoja wanasema hatua za tekinolojia hiyo ni kubwa katika kupambana na maambukizi ya UKIMWI.

Alama ya utambuzi na matumaini


Ute na mate kuchukuliwa kutoka mdomoni


 Wamesema anachotakiwa mtu kufanya ni kuchukuwa ute au mate yaliyopo katika kinywa chake kwa kutumia vifaa maalumu na kusugua katika fizi za juu na chini kisha kuweka ute huo katika kipimo ambapo baada ya dakika kati 20 na 40 jawabu hupatikana Kifaa hicho kinatarajiwa kupatikana kwa matumizi mwezi oktoba mwaka huu kwa wauzaji wa maduka ya rejareja zaidi ya 30,000 watakaokuwa na uwezo wa kuuza kifaa hicho ambacho kinaweza kuwa msaada wa kupunguza kufunga safari kwenda vituo vya afya kupima. 


Mamlaka ya chakula na madawa ya taifa hilo imesema ni kweli kifaa hicho kinauwezo wa kupima ukimwi lakini katika watu 12 watakaopima mtu mmoja kuna dalili ya kuwa na majibu chanya wakati hana virusi vya ugonjwa huo ambao ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vya watu wengi duniani.


  Ufanisi wa kipimo hicho
Lakini ufanisi wake ni kwa asilimia 92 wakati asilimia 8 inayobakia ndipo anaweza kupatikana mtu mmoja kuwa na majibu chanya wakati majibu yake ni hasi. Huwezo wa kifaa hicho unawekwa wazi kuwa unaweza kutambua aina mbili za virusi vya UKIMWI yaani HIV namba 1na HIV namba 2 ambavyo hapo awali ilikuwa vigumu kuweza kutambua kwa kipimo kimoja. 


Hali ya kwenda kwa wataalamu wa Afya kupata uhakika wa kupima haiepukiki kwani katika kila anayepima anashauriwa kuwaona wataalamu hao kuhakikisha suala hilo kwani si uhakikia wa asilimia100. 


Maoni juu ya utafiti mwingine 


Mtu akiwa ameshika kopo lenye vidonge vya kuongeza maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI Kulingana na utafiti mwingine uliofanya juu ya huwezo wa kipimo hicho unasema wazi kuwa kati watu 5000 wanaopima ni mtu mmoja tu anatapa majibu yasiyo sahihi kwa ungowa huo, ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Taifa hilo wanasema wanakubaliana nalo. 


Naye msemaji wa kampuni hii ya OraSure Technologies anasema bei ya kifaa hicho ni sawa na Euro 17 ambayo sawa na shilingi 3400 za Kenya na sawa na shilingi 34000 za Tanzania. Wakati huo huo Rais na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hii Douglas Michels anasema kifaa chao kitawasadia mno watu kupima na kutambua hali ya maambukizi ya UKIMWi kwa amani wakiwa nyumbani na wataklwenda kuwaona madaktari pale watakapo takiwa kufanya hivyo kwa matibabu zaidi. 


Kulingana na kituo cha Kupambana na Kujikinga na Mangojwa cha Marekani mpaka sasa nchi hiyo ina watu milioni1.2 wanaoishi na virusi vya HIV ambapo katika kila Wamerekani watano mmoja hatambui uzima wahali yake ya afya kama ana virusi hivi au la,huku kila mwaka watu 50,000 wanaambukizwa virusi vinayosababisha UKIMWI.

Posts Mpya

Comments Zenu

Hapa